Giving children the chance to choose

Children in Crossfire yapata ufadhili mkubwa kutoka UK Aid Direct ili kufikisha elimu bora ya awali kwa zaidi ya watoto 100,000 nchini Tanzania.

Shirika la Children in Crossfire, limepokea ruzuku kutoka UK Aid Direct, ambao ni mfuko maalum ufadhili kutoka Serikali ya Uingereza, kwa ajili ya kusaidia asasi za kiraia kupambana na umaskini. Lengo la msaada huu wa miaka mitatu ni kuwafikia watoto zaidi ya 100,000 wa umri wa miaka 5-6 kupitia uboreshaji madarasa ya awali yapatayo 700 Jijini Dodoma. Msaada huo pia una lengo la kuimarisha utekelezaji wa kazi za Children in Crossfire ngazi ya kitaifa na kutafuta mbinu itakayofaa kuanzisha na kuendesha kwenye jamii vituo vya malezi ya watoto wadogo wa umri wa kati ya miaka 3-5 ili katika miaka yao ya mwanzo maishani watoto wote wa Tanzania wapate elimu bora ya awali iliyo jumuishi.

Miongoni mwa kazi za shirika la Children in Crossfire ni kusaidia watoto miongoni mwa makundi ya pembezoni ulimwenguni ambao hukosa haki na mahitaji muhimu kwa sababu ya umasikini. Utendaji wetu unayaboresha maisha ya watoto wadogo nchini Tanzania na Ethiopia kwa kuinua kiwango cha huduma mbalimbali muhimu ikiwemo elimu, hususan wakati wakiwa na umri mdogo kabisa. Tunasaidia upataji wao wa elimu bora na ustawi wao kwa ujumla kwa sababu ya umuhimu wa uwekezaji kwa watoto katika umri huu unavyochangia kuwapatia fursa ya kutimiza ndoto zao za mafanikio maishani.

Mtendaji Mkuu wa Children in Crossfire, Richard Moore amesema, “kila mtoto anastahili kupata mwanzo ulio bora maishani mwake na elimu ya awali ni sehemu muhimu kuwezesha kutimiza hilo. Kwa kutumia uzoefu wa Children in Crossfire katika nyanja hii nchini Tanzania, mradi utafanikisha upatikanaji wa elimu ya awali iliyo bora na jumuishi kwa gharama nafuu.”

“Tutatekeleza mradi huu Jijini Dodoma tukianzia wilaya za  Kongwa na Chamwino. Kwa kupitia mifumo iliyopo, tutaandaa madarasa ya mfano yenye walimu tutakaowajegea umahiri wa kufundisha watoto wa umri mdogo. Kwenye shule hizo tutahamasisha uongozi wa shule pamoja na viongozi wa halmashauri husika kwa kuwapa mbinu na namna bora ya kusimamia utekelezaji ili uwe endelevu na kuwa  chachu ya uhawilisho kwenye shule na halmashauri jirani ili hatimaye shule zote  700 za serikali mkoani Dodoma ziwe na madarasa bora ya awali,” ameongeza Craig Ferla, Mkurugenzi Mkazi wa Children in Crossfire Tanzania.

Tunatoa shukrani za dhati kwa UK Aid Direct kwa kutuunga mkono na kuwekeza kwenye mradi huu ambao utatekelezwa kwa ubunifu wa kipekee nchini Tanzania; utekelezaji ambao usingewezekana bila msaada wao.

Masomo yanaendelea ndani ya darasa la awali lililoboreshwa kwa msaada wa Children in Crossfire, Shule ya Msingi Madizini, Morogoro, Tanzania.
Picha na: Christopher Myombo

Please Donate

Site by Thrive Web Designs |  Supported by the Secure Base Foundation
We are a registered charity in Northern Ireland (NIC101412) and The Republic of Ireland (CHY 20045517). Children in Crossfire is now also a registered 'Not For Profit' in the USA and is recognised as tax exempt under section 501(c)(3) of the Internal Revenue Code (EIN 46-2267122). We are developing Advisory Groups in Chicago and Boston to assist with a fundraising programme.
Select your currency
GBPPound sterling
EUR Euro